Tuesday, December 18, 2012

SAKATA LA MRISHO NGASA

Niliposikiliza kipindi cha michezo radio one stereo jumamosi, nilipata habari mbili zinazo leta mkanganyiko wa aina yake. Mrisho anasema hajui chochote. Rage anasema Ngasa anajua kila kitu. Hivi haya ni mazingaombwe au mchezo wa kuigiza?

Mimi hapo sijui tunaendeleza soka au tunadidimiza?

Thursday, December 13, 2012

LA MASIA -BARCELONA

Mafanikio yoyote hayaji kwa kukaa tu, au kutaka vitu rahisi. Watu wa ulaya wamejifunza maendeleo kuipitia nidhamu, bidii, utafiti elimu na uwekezaji. Tanzania tujifunze Barcelona. Barcelona wana timu za watoto katika umri mbalimbali (miaka 6 hadi 17). TFF iwekeze zaidi katika programu za watoto na vijana.