Monday, June 24, 2013

AZAM FC


Mechi kati ya Azam na FAR Rabat iliyofanyika Morocco



Timu ya Azam haina muda mrefu sana tangu imeanzishwa lakini mafanikio yake ni mfano wa kuigwa na timu kongwe hapa nchini kwetu. Ni mwaka 2007 tu walipoanza kushiriki ligi kuu ya Tanzania Bara na matunda yake tumeyaona. Tangu timu imeanza kushirikiligi kuu haijawahi kushuka daraja. Timu ina uwanja wake, kituo cha kuendeleza soka na timu za watoto na vijana.

Siyo ajabu kabisa kwamba kwa maraya kwanza kushiriki mashindano ya CAF imejizolea umaarufu mkubwa. Timu hii inabidi iwe mfano wa kuigwa kwa timu nyingine na hasa timu zetu za Simba na Yanga. Mpira wa mazoea na maneno tu hautatufikisha popote.


Tuesday, December 18, 2012

SAKATA LA MRISHO NGASA

Niliposikiliza kipindi cha michezo radio one stereo jumamosi, nilipata habari mbili zinazo leta mkanganyiko wa aina yake. Mrisho anasema hajui chochote. Rage anasema Ngasa anajua kila kitu. Hivi haya ni mazingaombwe au mchezo wa kuigiza?

Mimi hapo sijui tunaendeleza soka au tunadidimiza?

Thursday, December 13, 2012

LA MASIA -BARCELONA

Mafanikio yoyote hayaji kwa kukaa tu, au kutaka vitu rahisi. Watu wa ulaya wamejifunza maendeleo kuipitia nidhamu, bidii, utafiti elimu na uwekezaji. Tanzania tujifunze Barcelona. Barcelona wana timu za watoto katika umri mbalimbali (miaka 6 hadi 17). TFF iwekeze zaidi katika programu za watoto na vijana.