Mechi kati ya Azam na FAR Rabat iliyofanyika Morocco
Timu ya Azam haina muda mrefu sana tangu imeanzishwa lakini mafanikio yake ni mfano wa kuigwa na timu kongwe hapa nchini kwetu. Ni mwaka 2007 tu walipoanza kushiriki ligi kuu ya Tanzania Bara na matunda yake tumeyaona. Tangu timu imeanza kushirikiligi kuu haijawahi kushuka daraja. Timu ina uwanja wake, kituo cha kuendeleza soka na timu za watoto na vijana.
Siyo ajabu kabisa kwamba kwa maraya kwanza kushiriki mashindano ya CAF imejizolea umaarufu mkubwa. Timu hii inabidi iwe mfano wa kuigwa kwa timu nyingine na hasa timu zetu za Simba na Yanga. Mpira wa mazoea na maneno tu hautatufikisha popote.
No comments:
Post a Comment